JAMHURI YA
MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA
NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA
TAARIFA KWA UMMA
1.0 UTANGULIZI
Katika kukabiliana na Ajali za
Barabarani, ambazo zimekuwa zikitokea na kusababisha Vifo na Majeruhi, kutokana
na uzembe wa Madereva wasizingatia Sheria, Jeshi la Polisi, Kikosi cha Usalama
Barabarani nchini, linafanya Operesheni kali ya kuwakamata madereva
wasiozingatia sheria na kuwachukulia hatua kwa mujibu wa sheria, ikiwa ni
pamoja na kufungia leseni zao.
Operesheni
hii, sasa inafanyika Usiku na Mchana baada ya kubaini kuwa Madereva wa Mabasi
ya Abiria wanaendesha kwa mwendo kasi kufidia muda wa mchana ambao hawakimbii kutokana
na kudhibitiwa na Tochi za mwendo kasi kwa kuamini kuwa Usiku Tochi hazikamati
na Askari wa Usalama Barabarani hawapo Barabarani na hivyo hawawezi kukamatwa.
Operesheni
hii inafanyika sanjari na utekelezaji wa maagizo ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania aliyoyatoa hivi karibuni kuwataka madereva kutoendesha magari kwa
mwendo kasi, wakati wa ufunguzi wa barabara mpya huko Simanjiro.
Jeshi
la Polisi linatoa shukrani kwa wananchi kwa ushirikiano na kwa taarifa ambazo
wamekuwa wakitoa na kuweza kusaidia kuwakamata madereva wanaofanya makosa barabarani.
2.0
MAKOSA
YALIYOKAMATWA
Katika Operesheni inayofanyika, kwa
kipindi cha Wiki Moja, kuanzia tarehe 18
– 24/09/2017 tangu kuanza Operesheni hii jumla ya makosa 53,870 ya magari yamekamatwa. Idadi hii
ya makossa yaliyokamatwa na idadi ya makosa 53,053 yaliyokamatwa katika kipindi hiki cha wiki moja kuanzia
tarehe 11 – 17/09/2017 kabla ya Operesheni
haijaanza, inaonyesha kuwepo kwa ongezeko la jumla ya makosa 817 yaliyokamatwa. Hivyo ukamataji wa
makosa umeongezeka.
3.0
OPERESHENI
INAYOFANYIKA USIKU
Katika Operesheni inayofanyika Usiku
jumla ya Madereva Saba (7) wa Mabasi
yamekamatwa kwa kuendesha kwa mwendo kasi na hatarishi wa zaidi ya kilomita 90
kwa saa (90 km/hrs). Madereva walikamatwa waliwekwa mahabusu na kupelekwa
mahakamani ambapo walikiri kosa na kutiwa hatiani kulipa faini kati ya Tshs. 100,000/- hadi 300,000/-. Kwa kutiwa hatiani madereva hao wamepoteza sifa ya kuendesha
magari ya abiria kibiashara.
Kwa
Mamlaka niliyopewa kwa mujibu wa Sheria ya Usalama Barabarani, Tangazo la
Serikali Na.31 la mwaka 2015, Kanuni Na.5 ya Sheria hiyo, nafuta madaraja
“C” na “E” katika leseni za Madereva hao na hivyo hawataruhusiwa tena
kuendesha magari ya abiria na mizigo kibiashara kwa kipindi cha Miezi Sita (6) mpaka warudi darasani
wakasome, watahiniwe tena mpaka wafaulu ndipo warejeshewe madaraja hayo.
Madereva
hao ni:-
1. HAMAD SHABANI
SALUM, mwenye leseni Na.4001852854
2. KIJA
ALOYCE MAYENGA, mwenye leseni Na. 4001518000
3. ISACK
JOHN MBIJINA, mwenye leseni Na. 4000220395
4. HASSAN
ABASI SEMAZUA, mwenye leseni Na. 4001522366
5. STANLEY
JOSEPH MOSHA, mwenye leseni Na. 4000369436
6. ABDALLAH
HUSSEIN, mwenye Leseni Na. 4000482412 – huyu yuko Mahabusu.
7. SEMPUNDA
YUSUFU, mwenye leseni Na. 1-1980- 80006515226,
Aidha, dereva ISMAIL MOHAMED
NYAMI, mwenye leseni Na. 4000676285, aliyesababisha ajali tarehe 23/09/2017 iliyoua watu 2 na kujeruhi watu 42
Wilaya ya Nyasa, Mkoani Ruvuma, Dereva
MSEKA HERMAN SALUM, mwenye leseni 4000118648 aliyesababisha ajali tarehe 25/09/2017 iliyoua mtu 1 na kujeruhi wengine 25 katika eneo la Maganzo, Wilaya ya Kishapu, Mkoani Shinyanga na Dereva MALICK
HAMIDU HASSAN, mwenye leseni Na. 4000450337,
aliyesababisha ajali ya kugonga Ng’ombe usiku na kupinduka, tarehe 21/09/2017 na kusababisha Kifo cha mtu 1 na majeruhi 6, hao nao leseni zao zimefungiwa na hawataruhusiwa
kuendesha magari ya kubeba abiria.
Madereva
wote hao waliofungiwa leseni, Waajiri wao watajulishwa na hivyo hawaruhusiwi
kuendesha tena Mabasi. Pia Chama cha Wamiliki wa Mabasi (TABOA), Mamlaka ya
Mapato (TRA) na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA)
nao watajulishwa kufungiwa kwa leseni hizo kwa hatua zaidi.
4.0
MABASI YALIYOFUNGIWA
Kwa kusirikiana na SUMATRA, kwa
mujibu wa kifungu cha 15 cha Sheria ya
SUMATRA, jumla ya mabasi 11 ya Makampuni
mbalimbali yamefungiwa kutoa huduma ya kusafirisha abiria kwa makosa ya
mwendokasi mpaka wahakikishe vifaa vilivyofungwa katika Magari yao vya kudhibiti
Mwendo kasi vinafanya kazi. Makampuni hayo ya Mabasi tayari yamejulishwa
kufungiwa kutoa huduma.
5.0
MAFANIKIO YA OPERESHENI
Operesheni inaonyesha mwelekeo wa
kupungua kwa matukio ya Ajali, Vifo na Majeruhi. Kwa mfano kuanzia tarehe 18-24/9/2017 tangu Operesheni hii ianze, kumetokea jumla ya Ajali 37, Vifo 26 na Majeruhi 54. Ukulinganisha
takwimu hizo na kipindi kama hicho kuanzia tarehe 11-17/9/2017 kabla ya operesheni hii kuanza, ambapo zilitokea jumla
ya Ajali 66, Vifo 42 na Majeruhi 107
zinaonyesha kuwepo kwa Upungufu wa Ajali
29 ambazo ni sawa na 44%, Upungufu
wa Vifo 16 ambavyo ni sawa na
asilimia 38% na Upungufu wa Majeruhi 53 ambao ni sawa na asilimia 50%.
Aidha, Wananchi wengi wanaunga
mkono hatua zinazochukuliwa dhidi ya madereva wasiozingatia sheria na kutaka
operesheni hii iwe ya kudumu na endelevu.
Pia
hofu ya watu kusafiri kwa mabasi kutokuwa na uhakika wa kufika salama
imepungua. Wengi waliokuwa wameacha kupanda Mabasi kwa kuhofia kupata Ajali
sasa wameanza kupanda Mabasi
6.0
RAI
MADEREVA.
Madereva wazingatie sheria, wajenge
utii wa sheria bila shuruti, wasisubiri kushurutishwa, waache kuendesha kwa
mazoea na wabadilike. Wajue kuwa watakaofanya makosa barabarani watakamatwa palepale
na kuchukuliwa hatua kali ikiwa ni pamoja na kufungiwa leseni.
Aidha,
ieleweke kwamba, kwa makosa hatarishi, hatutatoza faini kwa njia ya Tozo la Notification. Tutawakamata
madereva, kuwaweka mahabusu, kuwapeleka mahakamani na kufungia leseni zao. Madereva
wajue kwamba kama udereva umewashinda, waache watafute kazi nyingine. Hatuwezi
kukubali kuona Watanzania wanaendelea kufa na kujeruhiwa kutokana na ajali
zinazosababishwa na madereva wazembe.
Pia
Madereva watambue kwamba operesheni hii ni ya kudumu na endelevu na itafanyika
muda wote, Usiku na Mchana. Wasidanganyike kuwa tochi zetu hazikamati usiku. Na kwamba Askari hawapo Barabarani. Tutawakamata
muda wote na kuwachukulia hatua kwa mujibu wa Sheria na kufungia Leseni zao
mara moja.
ABIRIA
Abiria watoe ushirikiano kwa
Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa pale wanapoona dereva anakiuka sheria. Abiria
wasikubali kufaulishwa na kupakiwa katika mabasi yaliyojaa.
Aidha,
Wasisubiri ajali itokee ndipo waanze kusema dereva alikuwa anaendesha kwa mwendo
kasi na kwamba walikuwa wamezidishwa katika mabasi.
Watafanya
kazi kwa kuzingatia Sheria, haki, maadili, huduma bora kwa mteja na
hawatabambikizia mtu makosa.
7.0
HITIMISHO
Dereva yeyote aliyepewa leseni ya
udereva bila kujali anaendesha gari ya aina gani, azingatie sheria vinginevyo atakamatwa
na kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa Sheria na leseni yake itafungiwa. Kwa
Operesheni hii na kasi hii dereva asiyetii Sheria hatabaki Salama.
“HATUTAKI
AJALI, TUNATAKA KUISHI SALAMA”
Imetolewa na:-
(FORTUNATUS
MUSILIMU)
KAMISHNA
MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI (SACP)
KAMANDA WA KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI (T)
TAREHE
28/09/2017
No comments:
Post a Comment