Saturday, 22 July 2017

KAMANDA MUSILIMU: HATUTATOA ELIMU BARABARANI KWA MAKOSA UTAKAYOYAFANYA


SACP FORTUNATUS M. MUSILIMU
KAMANDA WA KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI(T)

Kamanda wa Kikosi Cha Usalama Barabarani(T), Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Fortunatus Musilimu(SACP), amesema kuwa kwa madereva wanaofanya makosa wawapo barabarani na kutegemea kupewa Elimu barabarani wasitarajie hilo, akaongeza zaidi na kusema kuwa kama dereva unategemea ukapewe elimu barabarani basi ni bora ukaliacha gari lako nyumbani kwani anaamini kuwa madereva wote kabla ya kuanza kuingia barabarani wanakuwa wameshafundishwa Sheria na Kanuni za Usalama Barabarani.

Aidha Kamanda Musilimu amesisitiza kuwa hawatamuonea mtu wala Kubambikia Makosa wala Kesi, na kusisitiza pia Makosa ya Usalama barabarani ni Makosa kama Makosa mengine ya Jinai hivyo hawatasita kumchukulia hatua yeyote atakaekamatwa kwa Makosa ya Usalama Barabarani ili Kukabiliana na Ajali za Barabarani ambazo zinazidi kuchukua Uhai wa Watanzania wasio na hatia kwa uzembe watu wachache.

No comments:

Post a Comment