Monday, 10 October 2016

PICHA NA MATUKIO YALIYOJIRI KATIKA SIKU YA UZINDUZI WA WIKI YA NENDA KWA USALAMA BARABARANI KITAIFA MKOANI GEITA


Washiriki wa maonesho (waendesha bodaboda) wakiwa katika maandamano ya kuadhimisha Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani iliyozinduliwa katika Viwanja vya CCM Kalangalala,
mjini Geita leo. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “Hatutaki ajali tunataka kuishi salama”. Maadhimishjo hayo yalinduliwa na Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni. Katika hotuba yake Masauni aliwaagiza Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) kuyaondoa matuta yote yaliyopo katika Barabara Kuu na aliwataka madereva wote nchini kufuata sheria za usalama barabarani ili kupunguza ajali za kizembe.

No comments:

Post a Comment