Mgeni
rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa
Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto)
akimpa
zawadi ya Kombe la Ushindi wa kwanza Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Bunge jijini
Dar es Salaam, Veronica Innocent, ambaye alishinda nafasi ya kwanza katika
uchorani wa picha zinazoonyesha usalama barabarani ambayo zilipambanishwa
katika shule za Mkoa wa Dar es Salaam na Geita. Masauni aliyazindua Maadhimisho
ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani, ambayo yanafanyika Kitaifa, katika
Viwanja vya CCM Kalangalala, mjini Geita. Masauni katika hotuba yake aliwaagiza
Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) kuyaondoa matuta yote yaliyopo katika
Barabara Kuu na aliwataka madereva wote nchini kufuata sheria za usalama
barabarani ili kupunguza ajali za kizembe. Picha
zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
No comments:
Post a Comment