Mgeni
rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa
Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni (kulia),
akimsikiliza Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani kutoka Makao Makuu, Koplo
Faustina Ndunguru wakati alipokuwa anatoa maelezo jinsi magari mbalimbali yanavyovunja
sheria za barabarani. Katika hotuba yake ya ufunguzi wa maonyesho hayo
yanayofanyika Kitaifa mjini Geita, Mhandisi Masauni aliwaagiza Wakala wa
Barabara nchini (TANROADS) kuyaondoa matuta yote yaliyopo katika Barabara Kuu
na aliwataka madereva wote nchini kufuata sheria za usalama barabarani ili
kupunguza ajali za kizembe. Picha zote
na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
No comments:
Post a Comment