Mgeni
rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa
Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni akitoa hotuba ya
ufunguzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani alioizindua
Kitaifa mjini Geita leo. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “Hatutaki
Ajali, Tunataka Kuishi”. Katika hotuba yake, Masauni aliwaagiza Wakala wa
Barabara nchini (TANROADS) kuyaondoa matuta yote yaliyopo katika Barabara Kuu na
aliwataka madereva wote nchini kufuata sheria za usalama barabarani ili
kupunguza ajali za kizembe. Picha zote na
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
No comments:
Post a Comment